Kocha wa klabu Manchester United, Ole Gunnar anafahamu kuwa kitoweo chake kinaweza kupigwa teke wakati wowote. Aliyekuwa kocha wa Totenham Hotspurs, Mauricio Pochettino anatarajiwa kumridhi Ole atakapo pigwa kalamu mwishoni mwa msimu huu. Baada ya Manchester United kumsajili kiungo wa kireno, Bruno Fernades mwezi Januari huenda klabu hii ikkajirejeshea heshima yake hivi karibuni. Hatahivyo, kuna jina moja linalokosekana ugani Old Trafford ili maazimio hayo yatimie; Mauricio Pochettino
Mauricio Pochettino
Poch alikuwa kwenye mchuano baina ya klabu ya Leeds na
Brendford hivi maajuzi jambo lilozua mtafaruku pale nchini Uingereza hasa
kwenye kambi ya Klabu ya Manchester United. Pochettino alisaidia klabu ya Tottenham
Hotspurs kufika kwenye fainali ya Michuano ya klabu bingwa barani ulaya msimu
uliopita kabla ya kupigwa kalamu msimu huu.
Katika Michuano yake, Pochettino alipendea sana mfumo
wa 4-3-1-2. Alimpa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane majukumu ya kucheka na wavu kwa usaidizi wake
Dele Alli. Je, Klabu ya Manchester
united ina wachezaji wa hadhi yake Harry Kane pamoja na Dele Alli? Kwenye mfumo wake Pochettino alipendelea sana
kumtumia Mkenya Victor Wanyama kama kiungo wa kati kwa usadizi wake Harry
Wings
na Mousa Sissoko. Paul Pogba pamoja na Bruno Fernades wanauwezo huo?
Kwenye safu ya Ulinzi
Pochettino aliwapendelea walinzi wakibelgiji, Tobby Alderwield pamoja na
Jan Vertogen huku wakisaidiwa naye Danny
Rose pamoja na Serge Aurier. Kwa kuangazia kikosi cha Manchester United ambacho
kinaogozwa na beki ghali Zaidi ulimweguni, Harry Maguire kina uwezo wa hali ya
juu kuliko kikosi alichotumia Pochettino pale Totenham Hotspurs. Jambo hili
linawapa mashabiki wengi wa Manchester United Imani kuwa Pochetinho anauwezo wa
kuirejeshea Manchester United hadhi yake iwapo atapewa nafasi hio.
Tukilinganisha Vikosi hivi viwili ni kweli kwamba
Manchester United ya sasa ni moto wa kuotea mbali ila imekosa kocha wa
kuielekeza vilivyo. Je, Mauricio Pochettino ataibadilisha Manchester United?
@Albanus_10
No comments:
Post a Comment